Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Polisi mjini Mombasa walimtia mbaroni mshukiwa mmoja wa uwindaji haramu akiwa na pembe ya kifaru inayokisiwa kuwa na thamani ya shilingi milioni moja unusu.

Akithibitisha kisa hicho, naibu mkurugenzi wa shirika la huduma kwa wanyama pori Aden Alio alisema kuwa visa vya uwindaji haramu vinaonekana kuongezeka kila uchao na kukamatwa kwa jamaa huyo ni mojawapo wa juhudi zinazowekwa na shirika hilo kukabiliana na uwindaji haramu.

Wakati huo huo katika tukio lingine, jamaa mmoja anayekisiwa kuwa afisa wa polisi kutoka maeneo ya magharibi alipatikana na ngozi ya chui aliyokuwa akiuuza kwa shilingi elfu 80 mjini humo.

Mshukiwa huyu anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.