Share news tips with us here at Hivisasa

Idara ya polisi pwani imetakiwa kuwatia mbaroni washukiwa wa ugaidi badala ya kuwapiga risasi na kuwauawa kiholela.

Siku ya Ijumaa, mwenyekiti wa baraza kuu la waislamu katika kaunti ya Kilifi ,Bakari Ali, alisema kuwa idadi kubwa ya vijana wameuwawa kiholela kwa misingi kuwa ni magaidi Pwani.

Aidha, aliongeza kuwa imekuwa vigumu kwa maafisa wa polisi kutofautisha baina ya muislamu na gaidi.

Bakari alikanusha madai kuwa waislamu ambao wanafuga ndevu na kuvaa kanzu kubwa kuwa ni magaidi.

Aliwataka maafisa wa polisi kufanya uchunguzi wao kabla ya kuchukua hatua za kuwapiga risasi washukiwa hao.