Idara ya polisi katika eneo la Pwani imetakiwa kuwatia mbaroni vijana wanaowavamia wafuasi wa chama cha ODM huko Malindi.
Gavana wa Mombasa, Hassan Joho, amelaani visa va kuvamiwa kwa wafuasi wa ODM, na kusema kuwa hilo limetokana na joto la kisiasa za uchaguzi mdogo wa Malindi.
Akizungumza huko Malindi siku ya Jumatatu, Joho aliitaka idara hiyo ya polisi kuwataja mara moja na kuwachukulia hatua za kisheria wahalifu hao wanaodaiwa kupokea mafunzo ya jinsi ya kuvuruga uchaguzi huo mdogo uatakaofanyika mwezi Machi.
Aidha, alidai kuwa hiyo inaonekana kuwa njama ya wapinzani wao ambao wanaogopa kushindwa katika uchaguzi huo.
Wakati huo huo, Gavana wa Kilifi Amason Kingi ameishutumu serikali kwa kutowapa ulinzi kwenye mikutano yao ya kampeni, wakiitaja hatua hiyo kama kinyume cha sheria, huku akisisitiza kuwa wana haki ya kupewa ulinzi.