Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Maafisa wa polisi Veronica Gitai pamoja na Issa Mzee wanaodaiwa kumuuwa Kwekwe Mwandaza wamepatikana na kosa na mauaji bila kukusudia.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatano, jaji Martin Muya, alisema kuwa polisi hao hawakufanya uchunguzi wa kutosha ili kujua iwapo kulikuwa na watoto katika nyumba ya mshukiwa wa ujambazi waliyekuwa wanamsaka.

Aidha, aliongeza kuwa kulingana na sheria polisi hawaruhusiwi kufyetua risasi ama kupiga risasi watato kwa mujibu wa katiba.

Vile vile aliongeza kuwa washtakiwa hao walishindwa kuelezea mahakama iwapo walimuona mwendazake Kwekwe akishka panga huku akiwa na lengo la kuwakata.

Kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilindini kusubiri hukumu ya kifungo chao siku ya ijumaa.