Polisi mjini Mombasa wameanza msako dhidi wa washukiwa wawili wanaodaiwa kumuua mfanyabishara mmoja mjini humo siku ya Jumamosi.
Kulingana na walioshuhudiwa tukio hilo, mfanyibiashara Ali Athman mwenye umri wa miaka 23, alimiminiwa risasi na washukiwa wawili katika eneo la King’orani, Mombasa na kisha wakatoweka na pesa taslimu shilingi laki 400,000.
Akithibitisha kisa hicho, naibu OCPD wa Mombasa Patrick Njoroge alisema washukiwa hao walitoweka kwa pikipiki baada ya kutekeleza unyama huo.
Aidha, Njoroge alisema maafisa wa polisi tayari wameanza uchunguzi kuhusu kisa hicho na kuwa yeyote atakayepatikana na hatia atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mshukiwa alifarika muda mchache baada ya kufikishwa katika hospitali moja mjini Mombasa.