Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi eneo la Naikuro Manga kaunti ya Nyamira wameomba maafisa wa polisi kuimarishia usalama wao kufuatia ongezeko la visa vya wizi.

Wito huo umetolewa baada ya duka moja kuvunjwa usiku wa kuamkia siku ya Jumatano katika eneo la Naikuro. 

Wakizungumza siku ya Jumatano katika eneo la Naikuro, wakazi hao wakiongozwa na Elijah Mogere na Japhet Kondo walisema visa vya wizi vimekuwa vikiongezeka katika siku za hivi maajuzi katika eneo hilo huku wakihofia maisha yao na kuomba msaada wa maafisa wa polisi.

“Hapo mbeleni maafisa wa polisi walikuwa wakifanya patroli ya kupita usiku lakini kwanzia mwezi wa 6 mwaka jana hakuna patroli ya polisi imwewai fanywa katika eneo hili jambo ambalo limepelekea visa vya wizi kuongezeka,”  Elijah Mogere alisema.

Wakati huo huo, wakazi hao waliomba polisi kuanzisha uchunguzi kubaini ni akina nani walihusika katika wizi huo ili kutiwa mbaroni na kuchukuliwa hatua kali ya kisheria.