Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Raia 13 wa nchi ya Ethiopia wametozwa faini ya shilingi elfu 20 kila mmoja kwa kosa la kupatikana nchini kinyume cha sheria.

Siku ya Jumatatu, upande wa mashtaka uliambia mahakama kuwa kati ya Machi 11 na 13 Tekle Ababa, Alimayu Abeba na wengine walipatikana katika eneo la Likoni bila vibali mwafaka vya kuwa humu nchini.

Wote walikubali makosa hayo mbele ya hakimu mkuu Susan Shitub.

Mahakama iliwatoza faini hiyo ama kutumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani.