Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati mzozo wa ardhi ya shamba la Kiwambale eneo la Lunga Lunga.

Akizungmuza katika mkutano wa kisiasa mjini Mombasa siku ya Jumpili, Mwashetani alisema kuwa kamati ya bunge kuhusu ardhi ilifanya uchunguzi kuhusiana na shamba hilo na kusema kwamba linastahili kugawanyiwa wananchi kulingana na ripoti yao.

Mwashetani amemihiza Rais kulichukulia kwa uzito swala hilo na kuagiza kugawanywa ili wananchi wa eneo bunge hilo kupata ardhi ya kuishi.

“Tunamwomba Rais Kenyatta kutatua mzozo wa ardhi katika shamba la Kiwambale eneo la Lunga Lunga kama ilivyosuluhishwa katika shamba la Waitiki ili wakazi wa eneo langu pia wapata ardhi na hati miliki,” alisema Mwashetani.

Kauli ya Mbunge huyo wa Lunga Lunga imejiri baada ya wakazi wa Shamba la Waitiki eneo la Likoni kupata hati miliki za ardhi zilizotolewa na Rais Uhuru Kenyatta.