Share news tips with us here at Hivisasa

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuongeza siku za ziara yake katika eneo la Pwani kwa wiki moja baada ya kubaina kuwa kuna miradi mingine anahitajika kufungua rasmi kuanzia siku ya Jumatatu katika Kaunti ya Mombasa.

Kulingana na habari kutoka ikulu ya rais jijini Mombasa ni kuwa rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kufungua rasmi eneo la kuegeshwa boti aina ya Yacht, katika bandari kuu ya Mombasa.

Rais Uhuru amekuwa katika eneo la Pwani kwa siku saba sasa, na huenda hatua hii ni kujaribu kurudisha roho za wakazi wa kaunti ya Mombasa na hasa kujaribu kuwarai baadhi ya wakazi pamoja na viongozi ambao hawakufurahishwa na ziara ya rais ambapo wengi walionekana kummshtumu kiongozi wa nchi kuwa na mapendeleo.

Itakumbukwa kuwa Gavana wa Kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho tayari amemkosoa rais na kumtaja kuwa na mapendeleo ya kutoa miradi ya kimaendeleo kwa kupendelea baadhi ya maeneo ya Pwani.