Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Viongozi wa makanisa wana nafasi ya kupumua baada ya naibu Rais kuwaahidi kuwa sheria dhidi ya viongozi wa makanisa kujiepusha na kuomba pesa na usajili wa wafuasi wa makanisa yao kupitia vyombo vya habari hizo zitaangaliwa ili kuleta makubaliano ya pande zote mbili.

Naibu Rais William Ruto amesema kuwa hatua hiyo itashughulikwa na kuwataka wafuasi pamoja viongozi wa makanisa kuweka hofu yao mbali na kusema kuwa kila mtu ana haki ya kufanya mahubiri na kushiriki kwenye ibada bila kuingiliwa.

Akiongea siku ya Jumapili katika kanisa la Jesus Winners Ministry katika jiji la Mombasa, Ruto alisema kuwa yeye kama mmoja wa waumini wa kanisa atahakikisha kuwa sheria hizo mpya zinafanyiwa ukarabati na mabadiliko yakuwafaa Wakenya wote ambao wanapenda kuendeleza neno la Mungu.

“Mimi ni mmoja wa wale ambao walilelewa katika Sunday School na singependa kuona kanisa ikiwa chini ya udhibiti wa sheria kama hizo, lakini tutafanya juhudi kama serikali ili kuona kuna mabadiliko kwenye vifungo tata katika utaratibu huo mpya,” alisema naibu Rais.

Sheria hizo tata zinatarajiwa kuanza kufanya kazi baada ya miezi sita kufuatia tume ya mawasiliano nchini CA, kupitia kwa mkurugenzi mkuu wake Francis Wangusi ambaye amezipa pande husika; makanisa pamoja na vyombo vya habari kutilia maanani utarabu huo mpya chini ya miezi hiyo sita kabla ya kuanza kutekelezwa rasmi.