Share news tips with us here at Hivisasa

Naibu Rais William Ruto amezitaja siasa za viongozi wa upinzani kama siasa ambazo zimepitwa na wakati na kuwa hazina manufaa kwa maendeleo na ujenzi wa taifa.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumamosi katika hafla ya kuwapa hati miliki wakazi wa shamba la Waitiki eneo la Likoni, Ruto alimhimiza kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kukoma kumfuata kila mara na badale yake ajihusishe na mambo yake.

"Inakuhusu nini wageni wakinitembelea kwangu, inakuuma wapi ama ni kitu chako kipi kimetumika kuwakaribisha wageni hao? Bibi yangu Rachael hajalalamika kuwapikia wala sijakualika uje umsaidie kupika," alisema Ruto.

Kauli ya Ruto inajiri siku chache tu baada ya kiongozi wa upinzani Odinga kutaka achungzwe anakotoa pesa anazotumia kuandaa mikutano ya mara kwa mara na viongozi mbalimbali wa kisiasa nchini.

Siku ya Ijumaa wiki iliyopita, Ruto alikutana na wajumbe 12,000 kutoka Nyamira na Kisii nyumbani kwake Sugoi, Uasin Gishu, mkutano unaotajwa na upinzani kama wa kufuja pesa za mlipa ushuru.