Share news tips with us here at Hivisasa

Taasisi ya Demokrasia Kitaifa (NDI) pamoja na Muungano wa Wabunge Wachanga wa Kenya (KYPA), Alhamisi waliwapa vijana zaidi ya 100 kutoka eneo bunge la Gigil mafunzo kuhusu utaratibu wa ununuzi, utoaji kandarasi na mikopo kwenye serikali.

Ni katika kikao hicho cha mjini Gilgil ambapo Seneta Mteule Martha Wangari, ambaye pia ni mwanachama wa KYPA, alieleza haja ya kuwainua na kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kuwapa elimu wanayohitaji ili kupata nafasi za ajira kwenye serikali na kandarasi.

Seneta Wangari alisema itakuwa vigumu kwa vijana kunufaika na tenda zinazotoka kwa serikai bila yao kujua jinsi ya kuzipata, kuhifadhi pesa, kukopa na vile vile kuzitumia.

Alisema kwamba kama bunge, wamekuwa wakifanya kila jitihada kuhakikisha vijana hawatumiwi vibaya na wanasiasa, ambapo alisema imekuwa tabia ya mabwenyenye kuandikisha vijana wasio na masomo katika ufadhii Fulani, lakini pesa zinaingia kwenye bwenyenye huyo.

“Kama bunge la seneti na lile la kitaifa, tumejadili na kupitisha mswaada muhimu zaidi ulioletwa na mheshimiwa Johnson Sakaja unaoitwa Public Procurement Amemendment Bill, ambao utawapa nguvu zaidi vijana, akina mama na wanaoishi na ulemavu za kujiwezesha”.

Aidha alisema wamekuwa wakishinikiza rais Uhuru Kenyatta kuunda wizara ya vijana.

“Pia mimi nimeleta mswaada katika bunge la seneti unaoitwa Self Help Associations Bill ambao uko tayari kusomwa mara ya pili”.

Mswaada huo utadhibiti vijana wenye elimu kulaghai wengine wasio na elimu lakini ni wanachama.