Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Serikali inapanga kuajiri wahudumu zaidi katika hospitali zote nchini ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa.

Kauli hii ilitolewa siku ya Jumatatu na waziri wa afya nchini Cleopa Mailu jijini Mombasa, kwenye kongamano la maafisa wakuu katika wizara ya afya pamoja na wanakamati wa kamati ya afya katika bunge la kitaifa.

Mailu alisema kuwa ni jukumu la serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na serikali za kaunti kuboresha huduma za afya kote nchini.

Waziri huyo alisema kuwa wagonjwa wengi hukosa kuhudumiwa kutokana na uhaba wa wauguzi na madaktari katika hospitali za umaa nchini.

Aidha, alieleza wizara yake itaendelea kujitahidi kuweka zahanati tamba ili kusaidia wanawake wajawazito kujifungua, pamoja na kuwapa huduma hizo bila malipo.