Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Serikali ya Kaunti ya Mombasa imetakiwa kutenga sehemu maalamu kwa wavutaji sigara.

Ombi hili lilitolewa na mwakilishi mteule Mary Akinyi wa wadi ya Potriez.

Akizungumza siku ya Jumanne katika jengo la bunge la Kaunti la Mombasa, Akinyi alisema kuwa idadi kubwa ya wavutaji sigara huvuta sigara hizo jijini bila kujali wasiovuta sigara.

Akinyi alisema kuwa tabia hiyo inakera wananchi wengi wasiovuta sigara, na kuitaka serikali ya kaunti kutenga sehemu maalum ya wavutaji sigari.

Aidha, alisema kuwa wakaazi watakao patikana wakivuta sigara katika maeneo ambayo hayaruhusiwi wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisisitiza kuwa utafiti umesema kuwa watu ambao wanavuta hewa ya sigara ndio ambao wanaathirika sana na magonjwa.