Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Serikali ya Kaunti ya Mombasa imelaumiwa kwa kutojitahidi katika uzoaji taka katika eneo la Jomvu.

Wakaazi wa eneo hilo wakingozwa na Mauwa Juma, walilalamikia hali mbaya ya mazingira kutokana na mirundiko ya taka ambayo wanahofia huenda ikasababisha mkurupuko ya magonjwa.

Aidha, baadhi ya wanachama wa makundi ya kukusanya taka katika eneo hilo sasa wameitaka serikali ya kaunti kutafuta namna ya kusaidiana nao.

Makundi hayo yameitaka serikali ya kaunti kuwasaidia kupate vifaa vya kukusanya taka, iwemo magari ya kubebea taka.

Vijana hao walisema kwamba mara nyingi wao huwa katika hatari ya kuambukizwa maradhi kwasababu ya ukosefu wa vifaa.

Wamewataka wakaazi wa maeneo hayo kuchukua jukumu la msingi katika juhudi za kuimarisha usafi wa mazingira, na kushirikiana nao kila inapohitajika.

Vilevile, wameitaka serikali kutafuta mbinu za kukabiliana na taka kama vile nepi za watoto, ambazo wamesema huwapa changamoto kubwa katika kazi yao.