Serikali ya kaunti ya Nakuru imeshtumiwa vikali kwa kutojali maslahi ya wachuuzi.
Katika mahojiano ya kipekee, kiongozi wa wachuuzi mjini Nakuru Simon Ole Nasieku alisema kuwa tangu wafurushwe kutoka katikati mwa mji wa Nakuru wamepitia masaibu si haba.
Isitoshe ameongeza kuwa vibanda na vioski walivyojengewa na kaunti haviwezi kutumiwa kwani vingi vilijengwa juu ya bomba la maji taka ambapo ni athari kwa afya yao.
"Hapa ni shida tupu na sasa tunahofia mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu iwapo hali itaendelea hivi," Nasieku alisema.
Alisema wamejaribu kuzungumza na afisa mkuu wa afya ya umma Nakuru Samuel King'ori kuhusiana na swala hilo lakini hajapata jibu.