Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Serikali imeombwa kuweka matuta katika barabara kuu ya kutoka Kisii-Kilgoris ili kupunguza visa vya ajali ambavyo vinaendelea kushududiwa kila wakati katika barabara hiyo.

Hii ni baada ya ajali kushihudiwa kwenye eneo hilo siku ya Jumatano kutokana na kile wakazi wanasema ni magari kuendeshwa kwa kasi.

“Hakuna mwezi umewai kamilika bila ajali kufanyika katika barabara hii na kile ambacho tunashuku kinasababisha ajali hizi kila mara ni uendeshaji wa magari kwa kasi,” alisema Geoffrey Nyamisa.

“Kile tunahitaji kutoka kwa serikali hatuwezi nyamaza tukishuhudia wenzetu wakikufa kiholela na wengine kujeruhiwa tunaomba matuta kuwekwa katika barabara hili ,” alisema Martha Gesare mkazi mwingine

Wakati huo huo, wakazi hao walitishia kuandamana ikiwa serikali haitaweka matuta hayo kwa wiki mbili zijazo kulazimisha serikali kufanya hivyo .