Shirika la vijana wa Kiislam, KIMYA, limeishtumu serikali kwa kutoangazia vyema haki za kibinadamu na kuchangia hali ngumu ya maisha.
Mshirikishi mkuu wa shirika hilo katika ukanda wa Pwani Khamis Juma amesema kwamba kila mwananchi ana haki ya kutambua haki zake za kimsingi ili kuona kwamba zinazingatia.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatatu katika kongamano la hamasa kuhusiana na haki za kibindamu, Mwaguzo alisema serikali na baadhi ya viongozi nchini wamechangia dhulma nyingi za kimsingi kufuatia ongezeko la ukandamizaji wa haki za kibinadamu na ukiukaji mkubwa wa katiba ya nchi.
Aliongeza kwamba kama shirika la kijamii, wamechukua jukumu hilo kuwahamisisha wakazi il kufahamu zaidi jinsi ya kukabiliana na dhulma za kimsingi, unyanyasaji na ukiukaji wa haki za kibinadamu ili kuona kwamba maswala hayo yansitishwa.
"Serikali na viongozi humu nchini wamekuwa katika mstari wa mbele kukiuka haki za kibindamu kwa kuwadhulumu, kuwanyanyasa na kusababisha hali ngumu ya maisha katika jamii," alisema Mwaguzo.
Mwanaharakati huyo ambaye hutetea wa haki za kibinadamu eneo la Pwani ameahidi kuzuru mashinani na kuwahamasisha wakazi jinsi ya kutambua haki zao za kimsingi na kubadilisha uongozi wa nchi.