Serikali imetakiwa kuhakikisha kuna dawa za kutosha katika hospitali za Njoro.
Wito huu umetolewa na Johnson Mwamba, ambaye ametangaza azma ya kuwania kiti cha eneo binge la Njoro.
Akizungumza katika eneo la Industrial huko Njoro wakati wa hafla ya mchango wa fedha kusaidia matibabu ya mkazi kwa mmoja wa eneo hilo, Kinyanjui alisema kuwa vingi vya vituo vya afya eneo hilo havina dawa za kutosha.
"Ombi langu ni kwamba serikali isijenge tu vituo vya afya bali pia ihakikishe kuna dawa za kutosha," alisema Mwamba.
Wakati huo huo, mgombezi huyo ametoa wito kwa serikali kuhakikisha kwamba inatekeleza ahadi kwa mwananchi.