Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kitaifa imetakiwa kuwapa vijana wa Pwani ajira ya kudumu badala ya kuwaajiri katika mradi wa huduma kwa vijana NYS.

Akizungumza huko Malindi siku ya Jumanne, Gavana wa Mombasa Hassan Joho aliitaka serikali ya kitaifa kuwapa vijana kutoka ukanda wa Pwani ajira za kudumu katika mashirika ya kiserikali badala ya kuwaajiri katika mradi wa huduma kwa vijana, hatua aliyoitaja kama siasa za kuwahadaa Wapwani.

Joho aliongeza kuwa asilimia kubwa ya vijana katika eneo la Pwani hawana ajira, hali inayowafanya wengi kujiunga na mkundi ya kigaidi na utumizi wa mihadharati.

Kwa upande wake, mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba, alitoa changamoto kwa serikali ya kitaifa kutatua tatizo la ajira, kwa kusema umaskini ndio umesababisha idadi kubwa ya vijana kushawishiwa na mabwanyenye fulani ili kuyatekeleza maslahi yao.

Bedzimba alisema kuwa jambo hilo mwishowe husababisha vijana kukabiliwa na mkono wa sheria, huku baadhi yao wakilazimika kujitosa katika biashara duni zisizoweza kukimu mahitaji yao.