Naibu Rais William Ruto ameomba serikali za kaunti na serikali ya kitaifa kushirikiana pamoja kuleta maendeleo.
Akizungumza siku ya Jumapili katika uwanja wa Gusii, Ruto alisema serikali hizo zikishirikiana pamoja, basi wanachi wote watafaidika kimaendeleo.
Ruto alisema siasa za kugawanya wananchi kwa msingi ya kisiasa zimefika mwisho na kuomba wananchi wote kutokubali kugawanywa kwa msingi ya kikabila.
“Naomba serikali za kaunti na serikali ya kitaifa kufanya kazi pamoja ili wananchi kupata maendeleo ambayo wanahitaji kufanyiwa,” alisema Ruto.
Wakati huo huo, Ruto alikipigia chama kipya cha Jubillee upato na kuomba kila mwananchi kujiunga kwa chama hicho kwani chama hicho nia yake ni kuunganisha wakenya pamoja
“Sisi sote tunahitaji kuwa pamoja ninaomba mjiunge kwa chama kipya cha jubilee ambacho kinahitaji kuhakikisha tunakuwa na nchi moja ambayo ni Kenya ili maendeleo kushuhudiwa kikamilifu kwa kila mkenya,” aliongeza Ruto
Aidha, Ruto alipongeza majaji wa mahakama ya ICC kwa kutupilia mbali kutumika mashahidi waliojiondoa katika kesi dhidi yake na mshtakiwa mwenza Joshua Sang.
Ruto aliomba wananchi kuendelea kuwaombea ili kesi hiyo kutupiliwa mbali na kusema yeye yuko tayari kufanya maendeleo kwa wananchi wa Kenya.