Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa Timbwani, Likoni, wanalaumu tabia ya baadhi ya watu wenye mazowea ya kufanya mapenzi adharani katika ufuo wa bahari wa Shelly Beach eneo hilo.

Wakaazi hao wanasema tabia hiyo inaonyesha picha mbaya hasa ikizingatiwa kwamba ni ufuo unaopokea wageni mbalimbali kila wanapokuja kuzuru, na tabia hiyo inawaharibia sifa kwa wageni hao.

Akiongea na mwandishi wetu siku ya Jumatano, Osman Rashid, mkaazi wa eneo hilo, aliwaonya wenye tabia hiyo akisema pia inawaathiri watoto ambao mara kwa mara huenda kucheza katika ufuo huo.

“Sioni haja ya mtu kwenda kufanya mapenzi baharini tena adharani kabisa mchana, hata watoto wakicheza hapo wanaona kila kitu kinachoendelea na haileti picha nzuri kwa jamii," alisema Osman.

Inadaiwa watu hao huchukua fursa ya misitu inayopakana na ufuo wa bahari kutekeleza uovu huo na tabia hiyo imewakera zaidi wakaazi wanaosema wamewaharibia sifa kama mtaa wa likoni.

Aidha wanasema endapo watawakamata watu wakitekeleza vitendo hivyo watawashurutisha kutembea barabarani wakiwa uchi ili iwe funzo kwa watu wengine wenye tabia hiyo.