Shirika la uongozi bora la Centre for Enhancing Democracy and Good Governance CEDGG limeshtumu vikali hatua ya kunyimwa viza mkurugenzi wa maswala ya watoto Nakuru Bwana Kimemia. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Katika mahojiano, afisa wa mipango katika shirika hilo Masese Kemunche amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kwa ubalozi wa China kumnyima Bwana Kimemia viza ya kusafiri kutokana na changamoto ya ulemavu.

"Ni vibaya sana kwa ubaguzi kama huo na tunataka ubalozi wa China jijini Nairobi uombe msamaha," alisema Masese. 

Naye Mbunge mteule Emmah Mbugua anayewakilisha walemavu katika Bunge la Kaunti ameonyesha kughadhabishwa na hatua hiyo ya ubalozi wa China. 

"Ni mbaya sana kwa wanaoishi na ulemavu kubaguliwa kama ulivyofanya ubalozi wa China," alisema Mbugua. 

Hata hivyo, ubalozi huo haujatoa taarifa yoyote kuhusiana na swala hilo.