Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu, Human Rights Agenda (HURIA) katika kaunti ya Mombasa,  Yusuf Lule ametoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kuwachukulia hatua wote ambao wamehusishwa na sakata zima la ufujaji wa fedha za umma katika taasisi ya huduma kwa vijana (NYS) pasipo kuzingatia mirengo yao kisiasa.

Lule amesema kuwa uchumi wa taifa utazorota iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa dhidi ya wanaohusika katika sakata za ufisadi huku akieleza kuwa viongozi walioko mamlakani na wanashukiwa kuwa fisadi waondolewe haraka ili uchunguzi dhidi yao uanzishwe.

Mkurungezi huyo pia ameelezea kuwa kwa muda mrefu, Kenya imekuwa ikipoteza mabilioni ya fedha huku wanaohusika na kashfa za ufisadi wakiachiliwa huru bila kuadhibiwa na hata kutoregesha pesa hizo ambazo ni za wananchi.

“lazima serikali ifanye bidii na kuhakikisha kuwa watu wanaopatikana wakifuja pesa za umma wamechukuliwa hatua kali za sheria,” amesema Lule.