Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini (KNUT) Wilson Sossion pamoja na mwenyekiti, Mudzo Nzili wamechaguliwa tena kuhudumu kwa miaka mingine mitano ijayo.

Maafisa hao pamoja na kamati kuu ya KNUT, walichaguliwa bila kupingwa katika zoezi la uchaguzi wa chama hicho lililofanyika katika ukumbi wa Kasarani siku ya Ijumaa na kushirikisha walimu kutoka pembe zote za nchi.

Kwenye mtandao wake wa Twitter, Sossion alieleza furaha yake baada ya kukihifadhi kiti chake na kuwashukuru wanachama wa KNUT kwa kumchagua tena kwa kile amekitaja kama kuonyesha imani na utendakazi wake. Aidha, aliahidi kuendelea na juhudi zake za kuhakikisha kuwa walimu wanapata haki zao kwa kushinikiza serikali kutimiza maamuzi ya mahakama ya kuwapa nyongeza ya mshahara wa kati ya asilimia 50-60.

Kwa upande wao, walimu walioshiriki uchaguzi huo waliukashifu uongozi wa serikali ya sasa wakidai haijaangazia haki zao kama ilivyokuwa katika serikali ya Rais mstaafu Daniel Moi.