Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Spika wa bunge la kaunti ya Nyamira Joash Nyamoko amewahimiza wawakilishi wodi wa bunge hilo kuzingatia wakati wanapohudhuria vikao ili iwe rahisi kupitisha miswada muhimu kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Nyamoko alisema kuwa kufuatia kuchelewa kwa baadhi ya wabunge kuhudhuria vikao, upitishaji wa miswada muhimu umekuwa ukiathirika pakubwa.

“Kufuatia kuchelewa kwa baadhi ya wawakilishi wodi kufika bungeni ili kujadili miswada muhimu, bunge limekuwa na ugumu wakujadili miswada yenyewe kwa wakati unaofaa na kisha kuipitisha kwa manufaa ya wananchi," alihimiza Nyamoko.

Spika huyo aidha alionya kuwa afisi yake haitasita kuwachukulia hatua zakinidhamu wawakilishi wa maeneo wodi watakao kosa kufika bungeni kwa wakati na akahoji kuwa kufuatia kukaribia kutamatika kwa muhula wa kuhudumu wa bunge hilo, anatarajia kuwa wabunge watawajibika zaidi kwenye shughuli zao zakikazi. 

Alikuwa akihutubu alhamisi wiki jana kwenye hafla ya mazishi ya aliyekuwa mkurugenzi wa masuala ya uajiri katika bunge hilo Francis Onyoni kule Kegogi. 

"Katika mwaka ambao tunaumaliza hii leo (2015), asilimia kubwa ya wawakilishi wamekuwa wakichelewa kuhudhuria vikao vya bunge na kwa kuwa muhula wakuhudumu wa bunge unakarabia kutamatika ni tumaini langu kuwa wawakilishi husika watawajibika zaidi kazini."

"Afisi yangu haitasita kuwachukulia hatua kali zakinidhamu wale watakao endeleza tabia yakuchelewa na hata kukosa kuhudhuria vikao vya bunge," alionya Nyamoko.