Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwenyekiti wa chama cha madaktari nchini (KNUN), John Biiy amesema kuwa watahimiza wanachama wao kuchagua viongozi watakao leta maendeleo na kuboresha huduma haswa za afya. 

"Hatutachagua viongozi kwa msingi ya chama bali maendeleo na utendakazi wao," alisema Biiy. 

Akizungumza na wanahabari mjini eldoret siku ya Jumatatu, Biiy alisema kuwa viongozi walioko serikalini wanatumia fursa hiyo kujinufaisha binafsi. 

Aidha, Biiy amekashfu mswaada uliopitishwa na bunge ya kaunti ya Uasin Gishu wa kununua gari la kubebea maiti ambazo zitapeanwa katika hosiptali za wadi. 

"Mswaada kama huu hauto faidi mwananchi hasa ikizingatiwa kuwa hakuna dawa za kutosha hosiptalini, hii ni kuonyesha kuwa serikali ya kaunti inataka watu wakufe, ndio wawe wakitumia gari hizo, kuna hospitali haina dawa za kutosha," alisema Biiy. 

Mwenyekiti huyo alimwomba gavana kutotia sahihi mswaada huo iwapo hajatia sahihi.