Share news tips with us here at Hivisasa

Waendesha bodaboda mtaani maili sita wameapa kumuunga mmoja wao kuwania kiti cha uwakilishi wadi ya Kiamaina katika uchaguzi mkuu ujao. 

Wakiongea Jumamosi, wanabodaboda walisema kuwa wameamua kumuunga mkono mmoja wao ili wapate uwakilishi tosha. 

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Daniel Wachira wanabodaboda hao wameapa kufanya lolote ili kuhakikisha kuwa mmoja wao amechaguliwa.

"Kwa siku nyingi sana tumetumiwa vibaya katika kufanyia watu wengine kampeini lakini wakati huu tumeamua ni wakati wetu kupata moja wetu atakayetuongoza," alisema Wachira. 

"Tunataka mmoja wetu hapa awe MCA wetu hapa Kiamaina kwa kuwa tunajua atatuwasilisha vyema na kushugulikia mahitaji yetu," aliongeza.

Aidha wahudumu hao wa bodaboda walisema kuwa tayari wamemtambua mmoja kati yao watakaye mpigia debe ili achaguliwe. 

Walisema kuwa watafanya kila juhudi katika kumuuza mmoja wao kwa wapiga kura. 

Simon Mwangi ambaye ni mratibu wa mipango wa wanabodaboda hao alisema kuwa wanatarajia kupata uungwaji mkono kutoka kwa vijana na kina mama.

"Tumeweka mikakati ya kufanya kampeini na kuumuuza mgombea wetu kwa wapiga kura na tunahakika tutashinda," alisema Mwangi. 

"Wengi wetu ni vijana na tunataraji kuwa kina mama pia watatuunga mkono," aliongeza.