Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Zaidi ya vijana elfu moja kutoka eneo bunge la Mvita wamenufaika na ufadhili wa masomo kutoka kwa hazina ya CDF ya eneo bunge hilo.

Ufadhili huo chini ya mradi wa 'Skills Mitaani' unalenga kuwawezesha vijana kusomea taaluma mbali mbali za kiufundi kupitia ufadhili wa hazina ya ustawi wa eneo bunge hilo.

Akizungumza siku ya Jumanne, Mbunge wa eneo hilo Abdulswamad Nassir alisema mradi huo utaendeshwa kila mwaka lengo kuu ikiwa kuwaepusha vijana dhidi ya utumizi wa mihadari pamoja na kujihusisha na wizi wa mabavu.

Nassir alisema kuwa lengo lake kuu ni kuboresha sekta ya elimu katika eneo bunge lake ili vijana waweze kujitegemea pindi watakapomaliza masomo yao.

Aidha, aliwasihii vijana kuzingatia masomo na kujiepusha na janga la mihadharati na uhalifu jijini humo.

Zaidi ya shilingi milioni 25 zitatumika katika mradi huo wa kuelimisha vijana.