Wakulima kutoka eneo la Masaba Kusini kaunti ya Kisii watanufaika na mradi wa kaunti wa unaonuia kufufua kilimo kwa njia ya mikopo kwa wakulima.
Akiongea katika hafla ya kuwapa wakulima mwelekeo wa kilimo biashara siku ya jumatano, mkuu wa mikopo eneo la Baasi, Samwel Matonda amewataka vijana na akina mama kuchukua mikopo ya kaunti na ile ya serikali kuu ili kujiendeleza katika juhudi za kilimo humu nchini
"Vijana yatubidi kuchanuka katika nyanja za kilimo kupitia mikopo ya serikali ya kaunti na ya kitaifa ili tuweze kubuni nafasi za kazi badala ya kuhangaika tukitafuta kazi mijini," alisema Matonda.
Aidha, vijana waliohudhuria hafla hiyo wameitaka serikali kutoa vikwazo ambavyo wamesema huwafanya vijana wengi kutochukua mikopo hiyo.
Patroba Onkoba, mkulima wa nyanya na viazi alikiri kuwa ukulima ni changamoto kwake na kuihimiza serikali iwe na njia mwafaka ya kuwasaidia wakulima kupambana na changamoto hizo.
"Kuna nyakati za kiangazi na pia mafuriko ambayo ushababisha hasara kubwa na hutulazimu sisi kama wakulima kuhangaika kutafuta njia zingine za kulipa mikopo ya mashirika na ile ya serikali bila serikali kutuelewa na kufahamu shida hizo kupitia wizara ya Killimo," alisema.
Chifu wa eneo hilo bwana Thomas Getanda pia amewaahidi vijana ushirika wake hili kuimarisha miradi yao ya kilimo.
"Vjana yawapasa wajiunge na makundi ya kijamii hili kunufaika na mipango maalumu ya serikali," alisema chifu huyo.