Share news tips with us here at Hivisasa

Mwenyekiti wa baraza la wazee kanda ya bonde la ufa Gilbert Kabage ametoa wito kwa vijana wa kaunti ya Nakuru kwa jumla kujitokeza kwa wingi na kujisajili kama wapiga kura ili kuhakikisha wanashiriki haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.

Katika kikao na wanahabari mjini Nakuru, Kabage amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba wengi wa wananchi hukosa kushiriki shughuli ya kupiga kura na kisha baadaye wanalalamika kwamba uongozi uliopo umekosa kutekeleza wajibu wake.

''Mimi nataka wananchi wafahamu kwamba huwezi shiriki uchaguzi au kuwachagua viongozi kama hauna kitambulisho na kadi ya kupiga kura kwa hivyuo ni lazima wote tujiandikishe kama wapiga kura ndiposa tufaulu,'' Kabage alisema.

Wakati huo huo amesisitiza kuwa vijana ni nguzo muhimu kwa taifa hili na wanafaa kuhakikisha kwamba wana vitambulisho vya kitaifa.

Kwa mujibu wake,wengi wa vijana baada ya kujiandikisha kupata vitambulisho vya kitaifa hawatembelei afisi husika kuhakikisha kwamba wanapata vitambulisho hivyo.

''Inanikera sana ninaposikia kwamba kuna vitambulisho vimerundikwa katika afisi za vitambulisho kwa kuwa vijana hawajachukua hatua ya kwenda kuvichukuwa na ndiposa nawarai vijana wajitokeze na wachukuwe vitambulisho vya,'' Kabage alisema.

Matamshi yake yanajiri wakati ambapo joto la kisiasa limeanza kushamiri humu nchini huku kila mwanasisa akianza kuvuta kamba kwake.