Mamlaka ya Bandari nchini KPA imesema kuwa itawaajiri wafanyikazi zaidi ili kuiwezesha kuendesha shuguli katika behewa mpya waliopokezwa hivi majuzi.
Kaimu Mkurugenzi wa Bandari hiyo Catherini Mturi Wairi amesema kuwa hii ni habari njema kwa vijana kwa kuwa behewa hilo limeongeza nafasi za kazi kwa vijana wa kaunti ya Mombasa na wengine nchini.
Hata hivyo mkurugenzi huyo amesema kuwa maafisa wa bandari bado wako katika harakati ya kutathmini ni wafanyakazi wangapi watahitajika kabla ya kutangaza tarehe ambazo wataanza kuajiri.
Itakumbukwa kuwa bandari imekuwa ikiwafuta kazi wafanyikazi wengine huku wakiachishwa kwa maadai ya kutofuzu katika elimu ya kuwawezesha kufanya kazi bandarini.