Vikundi vya vijana katika eneo bunge la Nyaribari Masaba kaunti ya Kisii ambavyo havikutuma ombi la kukabidhiwa mikopo kutoka hazina ya Uwezo Fund vimehimizwa kutuma maombi.
Kulingana na mwenyekiti wa hazina ya Uwezo Fund katika eneo bunge hilo, Dennis Ongori alisema mikopo hiyo inatolewa ili kuhakikisha hali ya umaskini imepungua katika eneo hilo .
Akizungumza nasi, Ongori alisema hakuna haja kwa vijana kutegemea wanasiasa kwa kutaka pesa na kuwaomba kupata mikopo hiyo ili kufanya biashara na kujiendeleza kiuchumi.
“Vijana ambao wako katika vikundi na hawajatuma maombi ya kupata mikopo, nawaomba mufanye hivyo maana kuna pesa kwa ajili yenu ili tupunguze umaskini katika eneo hili letu,” alisema Ongori.
Ongori pia aliomba vikundi vingine vya akina mama kuendelea kuomba mikopo ili kujiendeleza katika eneo bunge hilo