Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Zaidi ya vijana 100 pamoja na makundi ya wanawake kutoka eneo bunge la Changamwe wamepokea mafunzo yatakayowawezesha kupata kandarasi za ujenzi kutoka hazina ya CDF.

Akizungumza katika ukumbi wa Aga khan Mjini Mombasa siku ya Jumanne, kwa niaba ya Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi, Mwakilishi wa mbunge huyo, Ibrahim Kilai, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia vijana pamoja na wanawake kuimarisha maisha yao kwa kupata kandarasi zinazotolewa na serikali.

Leeman Oduor, mmoja wa waliohudhuria mafunzo hayo, ambaye ni fundi, alieleza matumaini yake ya kujumuishwa na wanakandarasi wengine ili kuwepo kwa ushirikiano wa kufanya kazi pamoja.

“Nimefurahi sana kupata mafunzo haya kwa vile mafunzo kama haya yatasaidia pakubwa katika kutatua ukosefu wa ajira kwa jamii,” alisema Oduor.

Vilevile, aliwataka vijana kuwajibika katika maswala ya kimaendeleo na kuepukana na utumizi wa dawa za kulevya.