Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Vijana katika kaunti ya Nakuru wametakiwa kujihusisha sana na shuguli za kanisa haswa katika msimu huu wa sherehe za Krismasi.

Mwaniaji kiti cha uakilishi wadi ya kiamaina Regina Wamaitha amewataka vijana kuzingatia ushauri wanaopewa na viongozi wa kidini kama njia moja ya kujiepusha na maovu katika jamii.

Akiongea leo asubuhi alipotoa tenki ya maji kwa kundi moja la vijana mtaani Maili sita,Wamaitha alisema kuwa kanisa ni mahali salama kwa kila kijana haswa wakati huu ambapo maovu yameongezeka kwenye jamii.

“Kuna vijana wengi sana ambao sasa hivi wako nyumbani baada ya kukamilisha masomo na wengine kufunga shule na wengi wa vijana hao wanakosa ushauri mwema kwa kuwa wazazi wanashinda kazini na hii inapelekea vijana kujihusisha katika maovu kwenye jamii,” alisema.

“Kuna makanisa mengi sana ambayo yako wazi kuwapokea vijan wetu na kuwapa ushauri na kuwahusisha katika mambo mema na nataka kila kijana kusongea karibu na kanisa ili kujiepusha na maovu,” alisema.

Aidha aliyataka makanisa kuanzisha miradi itakayo wahusisha vijana kama vile kuandaa makongamano ya vijana ili kuwapa kitu cha kufanya wakati huu wa likizo.