Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Vijana katika kaunti ya Kiambu wameshauriwa kujisajili katika vikundi ili kunufaika na mkopo wa fedha kutoka hazina ya Uwezo badala ya kujiingiza katika siasa zisizo na msingi wowote.

Akiongea katika ibaada maalum ya kukukaribisha mwaka mpya katika kanisa la ACK Kiambu Askofu mkuu wa kanisa hilo , Timothy Ranji alisema vijana wanapaswa kujiepusha kutumiwa vibaya na wanasiasa na hata viongozi wa makanisa wasioaminika.

Badala yake aliwarai vijana kuchukua mikopo kutoka kwa hazina za kitaifa na kujihusisha na miradi ya maendeleo.

Wakati huo huo, Askofu Ranji aliwatahadharisha wakristo kote nchini dhidi ya kujiingiza katika madhehebu yasiyoaminika

Alidai kuwa Wakenya wengi wamepoteza mali na hata maisha yao kwa sababu ya kukosa kutambua madhehebu ya ukweli yenye kueneza injili ya Mungu. Kiongozi huyo wa kidini aliwashauri viongozi wa makanisa kukoma kuwalaghai waumini mali yao katika misingi ya injili potovu.