Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Vijana wameshauriwa kuasi mienendo isiyofaa ikiwemo anasa na badala yake kuzingatia maadili mema kila wakati.

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatatu katika eneo la Bismark, wakati wa maombolezo ya Brian Kariuki, mmoja wa vijana waliofarika kufuatia ajali katika eneo la Salgaa mkesha wa mwaka mpya, mwalimu na msahuri wa mmoja wa vijana hao, Kung’u Ndung’u, aliwataka vijana kuepukana na unywaji wa pombe.

Ndung’u alisema kuwa unywaaji pombe ulichangia kuangamia kwa vijana hao.

Matamshi hayo yaliungwa mkono na Gregory Mwangi, mwalimu wa dini katika parokia ya mtakatifu Monicah, ya kanisa katoliki section 58.

Mwangi alisisitiza umuhimu wa vijana kutafuta ushauri kutoka kwa wazazi na wakuu wao ili wapate mwelekeo maishani.

Mazishi ya marehemu Brian Kariuki ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya upili ya wavulana ya Solai yatafanyika siku ya Alhamisi katika Makaburi ya South Cemetry eneo la Manyani, viungani mwa mji wa Nakuru.