Share news tips with us here at Hivisasa

Viongozi wa vijana kaunti ya Nakuru wamewasuta viongozi fisadi na wanaoeneza ukabila. 

Philip Ng'ok kutoka bunge la vijana kaunti ya Nakuru alisema kuwa kaunti hiyo haitasonga mbele iwapo viongozi wa kaunti wataendelea kugawanya vijana kwa misingi ya ukabila. 

"Ni jambo la kusikitisha kwamba viongozi wa kaunti wanawatumia vibaya vijana kueneza ukabila," alisema Ng'ok. 

Aliongeza kuwa watazidi kuhamasisha vijana kujiunga na chama kipya cha Jubilee Party of Kenya ili kuleta umoja. 

"Tunaunga mkono chama kipya cha Jubilee maanake kitamaliza ukabila,"alisema Ng'ok.  

Ni matamshi yaliyoungwa mkono na Esther Mwai kutoka bunge la vijana kaunti ya Nakuru, akisema kuwa kaunti imekosa kutambua umuhimu wa vijana. 

Walisema kuwa vijana sharti wahusishwe katika maamuzi kwa mustakabali wa kaunti na taifa kwa jumla.