Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baraza la wazee katika Kaunti ya Mombasa limewaonya viongozi wa kisiasa dhidi ya kutoa matamshi yatakayovuruga amani nchini na kuleta mgawanyiko miongoni mwa wananchi.

Kwenye kikao na wanahabari jijini Mombasa siku ya Alhamisi, wazee hao wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo Mohamed Jahazi, walisema kuwa viongozi wanaotoa matamshi ya chuki na uchochezi wanapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kauli hiyo inajiri baada ya baadhi ya viongozi kudaiwa kutoa matamshi ambayo huenda yakazua vurugu walipokuwa katika mkutano wa kisiasa wikendi iliyopita katika Kaunti ya Kilifi.

Wakiangazia swala la uskwota katika eneo la Pwani, wazee hao waliunga mkono ada itakayotozwa wakaazi wa eneo la Likoni, watakaopewa hati miliki za Shamba la Waitiki.

Baraza hilo aidha limeitaka serikali kuu na ile ya kaunti kuzingatia kuimarisha sekta ya afya kwa kuongeza idadi ya wahudumu wa afya na vifaa vinavyohitajika katika vituo mbalimbali vya afya.

Pia waliitaka serikali kuimarisha usalama kwa kuhakikisha maeneo yanayokumbwa na ukosefu wa usalama yamewekwa taa za mitaani.