Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Vijana wa eneo la Pwani wanapaswa kuelezwa ukweli kuhusiana na misingi ya dini ili wasipotoshwe na magaidi na wala waliyo na itikadi kali.

Afisa wa maswala ya vijana katika Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la Huria, Chamosi Mwinyihijjah amesema kuwa iwapo vijana wataeliwa vyema dini na kuondoa mipaka ya imani kati ya Waislamu na Wakristu basi hapatakuwa na athari zozote za misimamo mikali.

Akizungumza eneo la Likoni mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Chamosi amesema kuwa inasikitisha kuona vijana wakijitosa katika maswala ya ugaidi na uhalifu huku viongozi wa kidini wakikosa kuchukua jukumu la kuwaongoza jinsi ilivyoangaziwa katika vitabu vitakatifu.

“Tunawasihi viongozi wa kidini kujitokeza na kuwaelimisha vijana kuhusu misingi ya kidini ili kuwaepusha kujiunga na makundi ya itikadi kali," alisema Chamisi.

Mwanaharakati huyo wa vijana hapa Pwani amewatahadharisha vijana kutohadaiwa msimu huu, siasa zinavyozidi kuchacha ili wasitumiwe visivyo na wanasiasa kwa maslahi yao binafsi.