Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Imewekwa bayana kuwa vuguvugu la maendeleo chapchap litaunga mkono Rais Kenyatta kwenye uchaguzi mkuu 2017.

Kauli hii ilitolewa siku ya Ijumaa na kiongozi wa chama cha TipTip, Kalembe Ndile alipoandamana na gavana wa Machakos daktari Alfred Muta walipokuwa wanazindua afisi ya maendeleo chapchap eneo la changanmwe, jijini Mombasa.

Ndile alisema kuwa serikali ya Jubilee imeonyesha mfano mzuri wa maendeleo na uongozi nchini kinyume na inavyodhaniwa na mrengo pinzani.

Aidha, aliongeza kuwa iwapo Cord haitapongeza hatua ya vuguvugu la maendele chapchap basi TipTip na maendeleo chapchap vitaungana na Rais kwenye uchaguzi ujao.

Vile vile, Ndile alisema kuwa gavana Mutua amefanya maendeleo ya kupigiwa mfano katika kaunti ya Machakos na kusisitiza kuwa mradi huo unafaa kuimarishwa kote nchini kwa manufaa ya wananchi.

Ndile ameusihi upinzani kushirikiana na serikali katika kuboresha uchumi na maendeleo ya taifa.

Wakati huo huo amewataka wanasiasa kutoingiza siasa zisizo kuwa na msingi kwenye miradi ya serikali.