Share news tips with us here at Hivisasa

Vyombo vya habari humu nchini vimetakiwa kuangazia mno haki za watoto ili jamii iweze kuzitambua na kuepusha dhuluma dhidi ya watoto.

Michael Sasi kutoka shirika la watoto la Mission in Action anasema kuwa iwapo jamii itaelimishwa ipasavyo basi visa vya dhuluma dhidi ya watoto vitapungua. 

Anasema kuwa hili litaafikiwa tu iwapo vyombo vya habari vitajitwika wajibu wa kuangazia mno haki za watoto. 

"Ombi langu tu ni kwamba vyombo vya habari viweze kujitwika jukumu hili na kuangazia zaidi kuhusu haki za watoto," alisema Sasi. 

Wakati uo huo, afisa huyo wa maswala ya watoto ameshtumu walimu wanaowadhulumu watoto shuleni. 

Kwa mujibu wake, serikali inafaa kujibidiisha na kuhakikisha sheria za kulinda maslahi ya watoto zinatekelezwa kikamilifu.