Afisa mkuu wa elimu katika kaunti ya Nakuru ametakiwa kuhakikisha kwamba waalimu wote wakuu wanafuata agizo la serikali la kuwachilia vyeti vya mtihani wa kitaifa kwa wanafunzi walioshindwa kukamilisha karo ya shule.
Himizo hilo limetolewa na chifu Stephen Koech wa eneo la Kaptembwo lililo viungani mwa mji wa Nakuru aliyekuwa akizungumza Ijumaa.
Chifu huyo aliteta kwamba hatua yao ya kuwaandikia barua waalimu wakuu kuwataka wawachilie vyeti hivyo haijakuwa ikizaa matunda .
Wakati huo huo, amewataka wazazi wote wa eneo bunge la Nakuru Magharibi ambao wanakabiliwa na matatizo ya wanao kutoenda shuleni kutokana na sababu moja au nyingine kuwasilisha malalamishi yao kwa machifu wa maeneo yao ili matatizo yao yaweze kutatuliwa .