Huku Wakenya wakisheherekea shamra shamra za mwaka mpya katika maeneo mbalimbali, wafanyibiashara wanaohudumu katikati mwa mji wa Mombasa wamelalamikia kupata hasara katika biashara zao.
Wakizungumza na wanahabari mjini Mombasa siku ya Ijumaa, wafanyibiashara hao wakiongozwa na Hussein Juma wamesema kuwa sikukuu ya kwanza ya mwaka mpya imewatoa matumani kufuatia kushuhudiwa kwa idadi ndogo ya wateja na kupelekea kurundikana kwa bidhaa zao.
Juma amesema kuwa iwapo idadi ya wateja itazidi kuwa haba mno hadi juma lijalo basi huenda wafanyibiashara hao wakaingia hasara zaidi huku wakiwahimiza wakaazi kujitokeza na kununua bidhaa zao hata za kitamaduni.
"Kwa kweli biashara msimu huu wa sherehe za mwaka mpya tumepata haasara kubwa sana kutokana na kusalia kwa bidhaa zetu kwani idadi ya wateja imekuwa ndogo sana ikilinganishwa na hapo awali," alisema Juma.
Lalama za wafanyibiashara hao zinajiri huku wadau wa sekta ya biashara wameahidi kubuni mbadali za kuimarisha sekta ya biashara nchini ili kuimarisha uchumi wa nchini unakumbwa na changamato.