Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wadau katika sekta ya utalii nchini, sasa wanapanga mikakati ya kusafiri mjini Miami nchini Afrika Kusini kujadiliana na wanachama wa muungano wa watalii katika bara la afrika jinsi watakavyouza utalii kimataifa.

Afisa wa Mawasiliano katika Halmashauri ya Bandari ya Mombasa KPA Hajj Maseno, alisema kuwa mikakati ya kuelekea mjini Miami inaendelea kukamilika kwani mipango hiyo itafufua juhudi za sekta ya utalii nchini.

Akizungumza na wanahabari katika Bandari ya Mombasa siku ya Jumanne, Hajj alisema kuwa wanachama wa muungano huo kutoka bara la Afrika ikiwemo, Dar es Salam, Mombasa, Afrika Kusini, Sychelles, Madagascar, Maputo na Namibia watatoa mwelekeo jinsi ya kuimarisha utalii katika nchi wanachama.

"Tunajiandaa kuhudhuria kongamano la kitalii litakaloandaliwa Miami katika muungano wa mwanachama wa utalii barani Afrika kuhakikisha kuwa tumekuza utalii wetu kimataifa ili kuinua viwango vya uchumi," alisema Hajj.

Kauli ya Hajj imejiri siku moja tu baada ya kuwasili kwa meli ya kitalii ya nane katika bandari ya Mombasa tangu mwezi Novemba ambapo meli hizo zilianza upya safari zao za kuzuru humu nchini.