Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wenye hoteli na mikahawa ya watalii eneo la Pwani wamependekeza kwa serikali kuu kuharakisha ukarabati wa barabara kuu ya kutoka Nairobi pamoja na barabara nyingine za kutoka uwanja wa ndege wa Moi ili kurahisisha usafiri wa watalii na wageni wengine kutoka uwanja huo.

Akiongea siku ya Jumapili na waandishi wa habari jijini Mombasa kwa niaba ya wamiliki wengine wa mikahawa na mahoteli, mkurugenzi mkuu wa Mombasa Beach Travellers Resort Fredrick Kiuru alisema kuwa barabara nyingi katika jimbo hilo la Pwani ambalo linategemea sana masuala ya utali kama kitega uchumi.

“Barabara mbovu ndicho chanzo cha wageni kuchelewa hasa wakati watalii wanapotoka kwenye uwanja mkuu wa ndege huwa wanakumbana na shida ya kusafiri kutoka eneo hilo kwa sababu ya kuwa na barabara ambazo zimeharibika, na kukiwa na barabara nzuri kutakuwa na usawa na uchukuzi ulio mzuri,” alisema afisa huyo.

Uwepo wa barabara mbovu katika maeneo mengi katika eneo zima la Pwani limekuwa swala ambalo hata wakazi pamoja na wafanyabiashara wamekuwa wakilalamikia kwa muda mrefu ambapo wameitaka serikali kuu pamoja na serikali ya kaunti kushirikiana na kuhakikisha kuwa barabara na miundomsingi kwa jumla inatengenezwa ili kushawishi watalii.