Mwenyekiti wa waendeshaji bodaboda mjini Kisii amewaomba waendeshaji hao kutobeba wateja zaidi ya mmoja na kuzingatia sheria za barabara kuzuia visa vya ajali.
Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa ajali nyingi husababishwa kupitia waendeshaji wa pikipiki ambao hubeba wateja zaidi ya moja, jambo ambalo ni kinyume na sheria za barabarani.
Akizungumza siku ya Jumanne mjini Kisii, Mice Mose aliwataka waendesha pikipiki kuzingatia sheria barabarani na kutobeba zaidi ya mteja mmoja ili kuzuia visa vya ajali kila mara.
“Naelewa kila mfanyibiashara hung’ang’ana kutafuta pesa lakini naomba waendeshaji pikipiki kuzingatia sheria na kutobeba wateja wawili hadi wanne kwa pikipiki moja jinsi imekuwa ikiripotiwa kila mara,’ alisema Mice Mose mwenyekiti wa bodadaboda mjini kisii
“Kuvunja sheria za barabara ni jambo ambalo halina msingi wowote sharti kila mwendesha pikpiki kuzingatia sheria za barabarani kwani hawaruhusiwi kubeba wateja kupita kiasi,” aliongeza Mose.
Wakati huo, Mose aliomba waendeshaji hao kujiandikisha kwa kwa vikundi ili kupata pesa za mikopo ili waimarishe biashara zao.