Wafanyibiashara katika Soko la Kongowea wameungana kwa pamoja kuwachagua wanachama wapya wa kamati la siko hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongozwa na aliyekuwa katibu mkuu wa wafanyibiashara wa soko hilo Bw Peter Nyagah, wafanyibiashara hao walikongamana siku ya Ijumaa wakiwa tayari kuchagua kamati itakayowasilisha maoni yao kwenye idara mbalimbali za serikali.

Hapo awali, Nyagah alilalamikia hatua ya baadhi ya viongozi waliokuwa serikalini kuwashawishi wafanyibiashara kuwachagua wanakamati bila kuzingatia utendakazi wao.

Akizungumza na mwandishi huyu kabla ya zoezi hilo kuanza, Nyaga alidai kwamba kuna sehemu ya ardhi ya soko hilo ambayo ilichukuliwa na viongozi wakuu waliokuwa kwenye serikali ya mpito, ambapo kwa sasa kumejengwa majumba ya kibinafsi yanayoendesha biashara ndani ya soko hilo.

Hata hivyo, kwa upande wao, wafanyibiashara hao walisema kuwa wako makini katika zoezi hilo kwani wanatabua kuwa baadhi ya viongozi hupenda kushinikiza zoezi kama hilo na kulifanya lisiwe lenye uwazi na huru.