Wafanyibiashara wa soko la Kenyenya wametishia kuandamana kulalamikia uchafu ambao umejaa na kutapakaa ili kulazimisha serikali ya kaunti kuondoa uchafu huo.
Kulingana na wafanyibiashara hao maafisa wa kaunti ya Kisii walitembelea soko hilo na kutoa ahadi ya kuondoa uchafu huo kwa miezi mitano iliyopita lakini hakuna chochote kimefanywa hadi sasa.
Wakizungumza siku ya Jumatano katika soko hilo, wafanyibiashara hao walisema wataandamana ili kutendewa haki kwa kuondolewa uchafu huo ambao umechafua mazingira katika soko hilo.
“Kwa juma moja lijalo tutafanya maadamano ili serikali ya kaunti ya Kisii kuondoa uchafu, na ikiwa haitafanya hivyo, tutaandaman,” alisema Evans Machoka, mwnabiashara.
Aidha, walisema hakuna vyoo kwa soko hilo na kulazimika kutumia vyoo vya kibnafsi, jambo ambalo wamelikemea na kudai kubaguliwa na serikali ya kaunti.
“Ni kama sisi hatuko katika serikali ya kaunti ya Kisii maana hatujawai nufaika na chochote kutoka kwa serikali,” alisema Francis Mokaya mwanabiashara mwingine.
Aidha, waliomba serikali ya kaunti kukarabati barabara za eneo bunge hilo ambazo walidai hazijatengenezwa na kaunti.