Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya Kaunti ya Kisii imeombwa kujenga vibanda katika soko lililofunguliwa hivi maajuzi mjini Kisii mkabala mwa duka la jumla la Turskys.

Wafanyibiashara hao walisema kuwa wanapata hasara kubwa kufuatia mvua inayoendelea kunyesha katika sehemu mbalimali nchini.

Waliomba Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae kuwajengea vibanda ili waweze kuendeleza biashara zao hata wakati wa mvua.

Akizungumza siku ya Jumanne mjini Kisii katika soko hilo, mwenyekiti wa wafanybiashara wa soko hilo Jeremiah Nyanamba, aliomba serikali ya kaunti kujenga vibanda ili wafanyibiashara wasiwe wanapata hasara wakati wa mvua.

“Tunaomba serikali ya kaunti kupitia Gavana James Ongwae kitujengea vibanda katika soko hili ili tusiwe tunapata hasara mvua inaponyesha,” alisema Nyanamba.

Aliongeza, “Soko hili lilifunguliwa na gavana wa kaunti ili wafanyibiashara wawe wanafanya biashara zao hapa na kujipatia riziki ya kila siku. Hata hivyo, tumeanza kushuhudia hasara nyingi kwasababu hatuna vibanda.”

Nyanamba alisema kuwa ujenzi wa vibanda utawafaa sana kwasababu wataweza kuendeleza biashara hata wakati wa mvua na kujiimarisha kibiashara na kimaisha